send link to app

Radio Mbiu


4.8 ( 7568 ratings )
Música
Desarrollador ASSOCIAZIONE RADIO MARIA A.P.S. ENTE MORALE RICONOSCIUTO
Libre

Radio Mbiu- Sauti ya Faraja ni Radio ya kibiashara lakini inayofanya vipindi vyenye kuwanufaisha
wasikilizaji kiroho na kimwili kwa pamoja, kuhabarisha na kuielimisha Jamii ya Watanzania
kulingana na mazingira, rika na nyadhifa mbalimbali.
Radio Mbiu- Sauti ya Faraja inapatikana eneo la Bunena Wilaya ya Bukoba Mjini Mkoani Kagera
na ofisi zake zinapatikana ndani ya viwanja vya Kanisa Mama la Jimbo Katoliki la Bukoba, ambalo
ni Kigango cha Familia Takatifu.
Radio Mbiu-Sauti ya Faraja ni Nyumba ya Ukarimu kwa watu wote bila kujali rangi, dini, umri,
kabila wala hali ya Mtu.
Radio Mbiu kwa sasa ina leseni ya hadhi Wilaya ambapo ina fursa ya kuwa na masafa matatu
katika kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kubadilisha hadhi ya leseni ya sasa.
Lengo la kwanza katika mwaka huu wa kwanza ni kuhakikisha kuwa inasikika katika Mkoa wote
wa Kagera kabla ya kujitanua na sehemu za mikoa ya karibu. Kwa sasa Radio Mbiu inasikika
katika wilaya za Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Muleba, Karagwe, Misenyi, na baadhi ya maeneo ya
wilaya za Kyerwa na Biharamulo. Eneo ambalo bado kufikiwa ni wilaya ya Ngara na baadhi ya
maeneo ya wilaya za Kyerwa na Biharamulo.